WAPENZI WA VALDARO (VALDARO LOVERS).

Kwa zaidi ya miaka 600 sasa, mabaki ya miili yao bado yanaendelea kulala usingizi wa milele yakiwa pamoja!.


Valdaro lovers (wapenzi wa valdaro) ndilo jina lililopewa kwa mabaki ya vijana wawili waliokuwa wapenzi.Mabaki haya yaligunduliwa mwaka 2007 katika kaburi la Neolithic karibu na kijiji cha Valdaro,Mantua-Italy.
Baada ya uchunguzi wa muda mrefu,imekuja kubainika kuwa wapenzi hawa walikuwa ni vijana chini ya umri wa miaka 20 wakiwa na urefu unaokaridiwa kufikia sentimita 157.Pamoja na kufanyika kwa uchunguzi wa kina kabisa wa kisayansi kubaini sababu za kifo chao na kwanini walizikwa kwenye kaburi moja wakiwa wamekumbatiana bado majibu hayajapatikana.Taarifa zilizopatikana kwa kusoma mabaki ya mfumo wa meno na mifupa ndiyo yanayotoa uhakika wa umri na urefu wao,lakini hayaelezi juu ya nini hasa ilikuwa sababu ya kifo chao
Ukiachilia mbali ushahidi huu wa kisayansi,baadhi ya maandiko ya historia yanasema kuwa wawili hawa walipendana sana katika taabu na raha.Walishirikiana katika mambo mengi sana na mambo yalipokuwa magumu waliamua kuanza kuchonga mawe (kuzama machimboni) ili kutengeneza vifaa vya mawe waweze kujikwamua kimaisha.Kumbuka kuwa watu hawa waliishi zama za mawe hivo uchongaji wa zana hizi ulikuwa ni miongoni mwa biashara muhimu kabisa kwa maisha ya binadamu.
Habari hizi za historia zinaweza kuwa na ukweli kwa kiasi fulani kwani ndani ya kaburi lao mwanamme alikutwa akiwa na mshale mkali kabisa wa kupasulia miamba shingoni mwake na mwanamke alikutwa na kiwembe kimoja kikali kilichotengenezwa kwa mawe kwenye nyonga zake pamoja na visu viwili vya mawe kiunoni pake.
Inasadikika kuwa walifunikwa na vifusi vya miamba na udongo wakiwa usingizini (huku wamekumbatiana) na kwa zaidi ya miaka 6000 wameendelea kubaki hivyo.Baada ya kugunduliwa kwao huko Italy mwaka 2007 waliendelea kuhifadhiwa bila kuwatenganisha.Wanabaki kuwa kielelezo bora kabisa cha mapenzi hasa kwa vijana.






Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog