KIDOKEZO #1


MAONYESHO YA MWILI WA GADDAFI

Baada ya kifo chake, serikali ya mpito iliyoongozwa na NTC iliuweka mwili wa Gaddafi kwenye freezer katika eneo la wazi la umma kati kati ya mji kwa ajili ya watu kujionea "ushahidi" kwamba Gaddafi ameuwawa.

Watu wengine walisafiri maelfu ya kilomita kutoka kila kona ya nchi ili kujionea "ushahidi huu".
Mwili wake uliwekwa hivyo pembeni ya mwili wa mtoto wake Mutassim mpaka siku ya Tarehe 24 October, 2011 ambapo uliondolewa kwa ajili ya maziko.



KIDOKEZO #2


KABURI LA GADDAFI

NTC waliuzika mwili wa Gaddafi jangwani katika eneo ambalo halijawahi kugundulika mpaka leo hii.
Mwili wa Gaddafi ulizikwa sambamba na mwili wa mtoto wake Mutassim Gaddafi pamoja na waziri wake Abu-Bakr Yunis Jabr.

Wote kwa pamoja walizikwa tarehe 25 October 2011.





KIDOKEZO #3


UNAFAHAMU CHEO CHA MUAMMAR GADDAFI?


Mara nyingi nikiwa "kijiweni" na zikianza stori kuhusu Gaddafi huwa napenda kuwauliza watu 'swali la kizushi' kama wanafahamu Gaddafi alikuwa ni nani nchini Libya!

Yawezekana wewe unafahamu lakini ajabu ni kwamba watu karibia 8 au 9 kati ya kumi ninao wauliza swali hili kama wanafahamu cheo cha Gaddafi, huwa wanajibu kuwa alikuwa ni Rais wa Libya!!

Kama ulikuwa haufahamu nikujuze kwamba Gaddafi hakuwa Rais wa Libya, wala hakuwa waziri mkuu, wala hakuwa mfalme.

Binafsi huwa napenda kusema kuwa cheo cha Gaddafi ni yeye binafsi ndiyo alikuwa anakielewa kiufasaha zaidi maana hata wananchi wake walikuwa hawakielewi sawia na lilipoanza vugu vugu moja ya vitu vigumu vilivyo kuwa vigumu kujieleza kwa wananchi ilikuwa ni cheo chake.

Gaddafi alipenda kujipambanua nafasi yake kama "Brotherly Leader and Guide of the Revolution of Libya" (au kwa kifupi "Brotherly Leader").

Chini yake kuna Rais, kisha kuna Waziri Mkuu na Baraza la mawaziri.

Gaddafi alikuwa anakanusha vikali kukihusisha cheo chake na "ufalme" bali alipenda kujipambanua kama "mtoa muongozo wa taifa" au "visionary" wa taifa.

Lakini mara kadhaa akiwa anafafanua cheo chake alipenda kutumia mfano wa Malkia Elizabeth wa Uingereza kuwa yeye ni "figurative head", ni kiongozi mkuu wa nchi lakini hausiki na shughuli za kuendesha serikali kila siku. Au tuseme hajajipa mamlaka ta kiserikali.

Hii kwa kiasi fulani ilikuwa inakinzana na uhalisia kwa kuwa ukweli ni kwamba Gaddafi licha ya mazuri yake yote, lakini alikuwa ameiweka Libya kiganjani mwake. Anachokisema yeye hakuna mwenye uwezo wa kukipinga na hakuna maamuzi yoyote makubwa yanayofanyika bila yeye kuafiki.

Pia Gaddafi alipenda kuelezea nafasi yake hiyo kama "Philosopher" wa taifa.
Hii inadhihirishwa na nadharia mpya ya kimfumo wa kiutawala aliotumia kuongoza Libya ambao mwenyewe aliuita "Jamahiriya" (state of the masses) ambao yawezekana mfumo huu wa kiutawala hautumiki sehemu nyingine yeyote zaidi ya Libya kipindi cha uhai wake.



MWISHO
Kuna mengi mno ya kuandika kuhusu maisha ya kanali Muammar Gaddafi lakini kwa makala hii nitaishi hapa...

Comments

Popular posts from this blog