Posts

Showing posts from May, 2019
Image
UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY HITIMISHO Kama ambavyo nilieleza asubuhi kwamba nitahitimisha makala hii kwa maneno machache sana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu ambazo zilinifanya hata kukatisha muendelezo wa makala hii siku zilizopita. Lakini naamini tutakuwa tumefikia lengo. Tuendelee… Katika ripoti ya The Warren Commision, ile kamisheni iliyoundwa na Rais Lyndon B. Johnson kuna mahala inasema kwamba kuna mtu ambaye alijitambulisha kama "Clay Bertrand" alimpigia simu Dean Andrews Jr. ambaye alikuwa ni mwanasheria wa kujitegemea kwenye jimbo la New Orleans kumtaka apande ndege kwenda Dallas kumtetea Lee Harvey Oswald. Lakini wajumbe wa Warren Commision wanadai kwamba walihangaika mno bila mafanikio na hawakujua huyu "Clay Bertrand" ni nani na wakafanya hitimisho kwamba hili halikuwa jina halisi bali ni 'alias' ambayo ilitumiwa tu na huyo mtu. Ilipofika mwaka 1967 mwezi March… mwanasheria wa serikali wa New Orleans wa kipindi hi
Image
UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY Siku hii Rais Kennedy alikuwa amefika jimboni hapa kwa ajili ya ziara fupi maalumu na mahsusi ili kwenda kusukuhisha mvutano uliokuwepo kati ya wanachama wa Democrat Bw. Raph Yarborough na Don Yarborough dhidi ya Gavana wa Republican Bw. John Connally (nitaeleza huu mgogoro ulihusu mini). Safari hii ya Rais Kennedy kutembelea jimbo la Texas ilikuwa ilikuwa imepangwa na kukubaliana tangu mwezi June ambapo Kennedy, makamu wa Rais Lyndon B. Johnson na Gavana Connally walipokutana kwenye kikao mwezi June mwaka huo 1963. Safari hii ya Kennedy jimboni Texas ilikuwa na malengo makuu matatu. Mosi, alikuwa anataka kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kuongeza michango katika mfuko wa kampeni. Pili, alikuwa anaweka mkakati kwa ajili ya uchaguzi uliokuwa unafuata mwaka mmoja baadae, yaani mwezi Novemba mwaka 1974. Na tatu, Kennedy alikuwa anataka kujiimarisha zaidi katika jimbo la Texas kwa kuwa alipata ushindi mwembamba sana jimboni hapo na alikuw
Image
The Richest Man In Africa: Kila Utajiri Una ukafiri nyuma yake SEHEMU YA TATU Kwa wasomaji wa makala zangu naamini watakuwa si wageni kwa mtindo wangu wa uandishi ninaopendelea mara kadhaa kwa kuianza simulizi kuanzia mwishoni au katikati na kisha kuchambua mwanzo wa sakata zima na hiki ndicho nakusudia hasa kukifanya katika makala hii. Katika sehemu zilizopita nilieleza namna ya mazingira ambayo Mzee Kabila aliuwawa na pia nimegusia kiduchu kuhusu washirika wa mauaji hayo. Lakini pasipo kutoka nje ya mstari na kusahau lengo, makala hii si mahususi hasa kuchambua historia au mgogoro wa Congo bali ni utetezi wangu juu ya hoja ambayo najaribu kuijenga kuhusu mtu ambaye ni tajiri zaidi barani afrika lakini kamwe huwezi kukuona akitajwa katika majarida ya kuorodhesha matajiri kama Forbes na Forbes Africa. Kama ambavyo nilianza kujenga hoja yangu juu ya ushawishi alionao katika ukanda huu wa nchi za maziwa makuu na namna ambavyo ana uwezo wa kuratibu matumizi ya rasilimali katik
Image
The Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yake SEHEMU YA PILI Katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii nilieleza juu ya kifo cha kamanda Anselme Masasu aiyehukumiwa na kupigwa risasi mbele ya rafiki yake na msaidizi wake Antoine Ngalamulume msituni karibu na mji wa Lubumbashi. Pia nilieleza juu ya kikao cha siri kilichofanyika katikati ya jiji la Kinshasa kati ya raia a Lebanoni na mfanyabiashara maarufu wa almasi Bwana Bilal Hritier aliyekutana na mwakilishi wa ‘kigogo’ kutoka Rwanda na George Mirindi ambaye alikuwa ni moja kati walinzi wakuu wa Rais Laurent Kabila. Kisha nikaeleza juu ya mabadiliko ya biashara ya madini ambayo Rais Kabila alikuwa anayafanya kutoka kuwa na ‘deal’ ya moja kwa moja na Heritier mpaka kuwapa kampuni ya kiisrael iitwayo IDI Congo ‘monopoly’ ya biashara ya almasi ndani ya nchi ya Congo. Lakini pia nilieleza juu ya mipango ya Rais Laurent Kabila kwa kushrikiana na Israel kutaka kutengeneza kitengo maalumu cha intelijensia
Image
The Richest Man in Africa: Nyuma ya kila utajiri kuna ukafiri SEHEMU YA KWANZA Wanasema ukosefu wa rasilimali unakufanya uchakate ubongo zaidi. Hii yaweza kuwa kweli katika ngazi ya mtu binafsi na hata taifa kwa ujumla. Unaweza kujipima binafsi namna ambavyo ukiwa 'umechacha' mbongo yako inavyochakata mawazo ili uweze kupata kile ambacho unakihitaji. Vivyo hivyo katika ngazi ya taifa, ukosefu wa rasilimali unaweza kufanya taifa kuwa na mipango madhubuti zaidi na hari zaidi ya kujipatia maendeleo. Mfano mzuri wa kuthibitisha hili ni nchi kama Singapore. Kanchi kadogo kabisa ambacho hakajajaaliwa rasilimali yeoyote, yamenyimwa mpaka ardhi na inawabidi 'kutengeneza' ardhi kutoka baharini kwa ajili ya matumizi yao. Singapore ambayo haina hata maji 'matamu' yasiyo na chumvi kutosheleza mahitaji ya wananchi hivyo inawapasa kununua maji kwa mabilioni ya lita kwa mwaka kutoka nchi jirani ya Malaysia ambapo wameunga bomba la kipenyo kikubwa kuingiza maji nchini
Image
KIDOKEZO #1 MAONYESHO YA MWILI WA GADDAFI Baada ya kifo chake, serikali ya mpito iliyoongozwa na NTC iliuweka mwili wa Gaddafi kwenye freezer katika eneo la wazi la umma kati kati ya mji kwa ajili ya watu kujionea "ushahidi" kwamba Gaddafi ameuwawa. Watu wengine walisafiri maelfu ya kilomita kutoka kila kona ya nchi ili kujionea "ushahidi huu". Mwili wake uliwekwa hivyo pembeni ya mwili wa mtoto wake Mutassim mpaka siku ya Tarehe 24 October, 2011 ambapo uliondolewa kwa ajili ya maziko. KIDOKEZO #2 KABURI LA GADDAFI NTC waliuzika mwili wa Gaddafi jangwani katika eneo ambalo halijawahi kugundulika mpaka leo hii. Mwili wa Gaddafi ulizikwa sambamba na mwili wa mtoto wake Mutassim Gaddafi pamoja na waziri wake Abu-Bakr Yunis Jabr. Wote kwa pamoja walizikwa tarehe 25 October 2011. KIDOKEZO #3 UNAFAHAMU CHEO CHA MUAMMAR GADDAFI? Mara nyingi nikiwa "kijiweni" na zikianza stori kuhusu Gaddafi huwa napenda kuwauliza watu 's
Image
KANALI MUAMMAR GADDAFI (1942 - 2011) SEHEMU YA TATU Moja ya michoro ya kumkejeli Gaddafi iliyochorwa mjini Bayda baada ya vurugu kushika kasi nchi nzima Katika sehemu iliyopita nilieleza namna ambavyo vugu vugu la maandamano jinsi lilivyoibuka na kukolea katikati mwa mwezi February mwaka 2011. Katika sehemu hii ya tatu nakusudia kuandika zaidi kuhusu namna ambavyo vikundi vya waasi viliibuka na hatimaye kumuondoa Gaddafi madarakani. Tuendelee… Baada ya vugu vugu kupamba moto hasa na maandamano kukolea karibia nchi nzima ya Libya, na hatimaye kundi kubwa la polisi na wanajeshi kuasi, taratibu ikaanza vugu vugu la kupinga Gaddafi kwa kutumia silaha badala ya maandamano pekee. Mwanzoni kabisa mwa vugu vugu hili la kutumia silaha, vikundi vya wapiganaji vilikuwa vinaundwa na raia wa kawaida waliojitolea kushika mtutu. 'Volunteers' hawa waliojitolea kupigana walikuwa wengi wao wanatoka kada za ualimu, wanafunzi, na wafanyakazi katika visima vya mafuta. Taratibu