VIWANDA VYA KUCHAKATA TAARIFA.?? Kama mtu akikuuliza maswali yafuatayo, unajisi majibu yako yatakuwa ni yapi? 1. Jengo la picha namba moja unahisi linahusiana na nini? 2. Jengo la picha namba mbili ni nyumba ya kuishi au hoteli? Nina amini kabisa majibu mengi yatakuwa kama ifuatavyo… 1. Jengo namba moja ni kiwanda… na inawezekana ni kiwanda kinachohusiana na masuala ya nishati au kemikali. 2. Jengo kwenye picha namba mbili ni aina ya hotel ya nyota tano. Majibu mengi yatakuwa yanafanana na hayo hapo juu na kwa kawaida utakuwa sahihi kabisa… isipokuwa tu hautakuwa umepatia hata nusu ya jawabu. Picha zote mbili ni picha za kituo data (data center). Katika karne ya 18, 19 na 20 wafanyabiashara wenye mitaji mikibwa na makampuji walikuwa wanajenga majengo makubwa ya viwanda. Na wale ambao walikuwa mahiri kwenye uanzishaji na uendeshaji wa viwanda ndio ambao walikuwa wanashamiri kwa kipato na hatimaye kuwa matajiri. Matajiri wote wakubwa wa miaka hiyo… toka kwa wanasa...