VIWANDA VYA KUCHAKATA TAARIFA.??


Kama mtu akikuuliza maswali yafuatayo, unajisi majibu yako yatakuwa ni yapi?
1. Jengo la picha namba moja unahisi linahusiana na nini?
2. Jengo la picha namba mbili ni nyumba ya kuishi au hoteli?
Nina amini kabisa majibu mengi yatakuwa kama ifuatavyo…
1. Jengo namba moja ni kiwanda… na inawezekana ni kiwanda kinachohusiana na masuala ya nishati au kemikali.
2. Jengo kwenye picha namba mbili ni aina ya hotel ya nyota tano.

Majibu mengi yatakuwa yanafanana na hayo hapo juu na kwa kawaida utakuwa sahihi kabisa… isipokuwa tu hautakuwa umepatia hata nusu ya jawabu.
Picha zote mbili ni picha za kituo data (data center).
Katika karne ya 18, 19 na 20 wafanyabiashara wenye mitaji mikibwa na makampuji walikuwa wanajenga majengo makubwa ya viwanda. Na wale ambao walikuwa mahiri kwenye uanzishaji na uendeshaji wa viwanda ndio ambao walikuwa wanashamiri kwa kipato na hatimaye kuwa matajiri.
Matajiri wote wakubwa wa miaka hiyo… toka kwa wanasayansi na wagunduzi kama Thomas Edison mpaka kwa mabepari kama John D. Rockefeller... utajiri wao ulitokana na umahiri wao wa kuanzisha na kuendesha viwanda.
Lakini katika hii karne yetu ya ishiri na moja… utajiri unatengenezwa kutokana na umahiri wa mtu au kampuni kuchakata na kutumia taarifa.
Leo hii kampuni zenye mitaji mikubwa zaidi ni zile ambazo zinahusika na masuala yanayogusa taarifa. Mfano leo hii tukiangalia kampuni kumi yenye mitaji mikubwa zaidi duniani… kampuni tano za kwanza zote zinahusika na masuala ya taarifa.
1. Apple
2. Google
3. Microsoft
4. Facebook
5. Amazon
6. Berkshire Hathaway
7. Exxon Mobile
8. Johnson & Johnson
9. JPMorgan Chase
10. Tencent Holdings
Kampuni hizi za teknolojia za mawasiliano umahiri wao na ubunifu wao wa kuchakata taarifa ndio umewafanya kuwa 'giants' wa biashara za karne hii ya ishirini na moja.
Lakini swali moja muhimu ambalo mara myingi haliangaliwi ni namna gani kampuni hizi zinaweza kuhimili ukubwa na wingi wa taarifa hizi zinazopita mikononi mwao kila sekunde.
Kwa mfano Facebook ina watumiani bilioni 1.37 kila siku. Watu hawa wanatumiana jumbe za maandishi, picha, video na pia wanatumia kitufe cha "Like" na kadhalila. Ni namna gani ambavyo Facebook inahimili ukubwa huu wa watumiaji na data kila siku??
Picha hizo hapo juu ni moja wapo ya majengo ya Facebook ambayo yanahifadhi 'server' za facebooks (Data Center). Kampuni ya Facebook ina Data Center kama hizi kadhaa maeneo mbali mbali duniani. Kwa mfano hii pekee pichani iliyoko Priveville, Jimboni Oregon nchini Marekani imegharimu kiasi cha dola za kimarekani Milioni 450 (kama shilingi Trilioni moja ya Kitanzania) kuijenga mpaka kukamilika.

Jengo hili lililojengwa kwenye shamba lenye ukubwa wa futi za mraba 350,000 (kama viwanja vitatu vya mpira wa miguu) hapa ndipo kila kitu ambacho unakifanya kwenye mtandao wa Facebook kinahifadhiwa.
Jengo hili linatumia umeme wa Megawatt 30 na ina majenereta makubwa ya umeme wa akiba 14 ambalo kila moja lina uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawatt 3 kama ikitokea umeme wa kawaida ukizimika.
Jengo hili limejengwa kwa mfumo maridhawa ili kuwezesha ufanisk wake wa kutenda kazi. Kwa mfano, jengo lenye server kubwa kiasi hiki lazima litakuwa linazalisha joto kubwa kutokana na server hizo kufanya kazi. Kwa hiyo lazima kuwa na mfumo maridhawa wa kuratibu kiwango cha joto katika jengo kama hili.
Kwa mfano kompyuta ya kawaida inaratibiwa joto lake na 'hit sync' yenye ukubwa wa kufanana na kasha la kiberiti. Jengo hili la Facebook joto lake linaratibiwa na mfumo complex wa uliopo kwenye paa la jengo ambao una mfumo wa hewa wa kutosha vyumba saba vikubwa.
Hewa inanyonywa kutoka angani, kisha inachujwa na kuwekwa ubaridi mkali na baada ya hapo inaingia kwenye 'chumba' maalumu ambacho inapashwa tena joto na kuongezewa/kupunguzwa unyevu kidogo mpaka kufikia kiwango ambacho ni sahihi kuingia kwenye 'hall' lenye severs.
Upande mwingine kuna 'feni' kubwa ambazo zinapuliza muda wote ili kuondoa hewa hii ilivyoingia kila baada ya muda fulani ilinkupishwa hewa nyingine 'fresh' kuingia.
Kutoka na ukuaji wa haraka kila siku wa mtandao huu… server mpya zinawasili kwenye vituo hivi kila siku. Facebooks wenyewe wanaeleza kuwa kwa sasa kwa mfano kituo hiki cha Prineville pekee kina hifadhi zaidi ya Pentabyte 700 za picha na video za watumiaji wa facebook (Pentabyte moja ni sawa na Terabyte 1000 kwa hiyo hii ni sawa na kusema kuchukua Terabyte 1000 zidisha kwa 700).

Moja ya Jenereta 14 za Disel za umeme wa dharura... kila jenereta ina uwezo wa kuzalisha 3 Megawatt za umeme


Sehemu ya mfumo wa feni zinazotumika kusukuma hela iliyonyonywa kutoka angani na kuipeleka kwenye hall lenye servers.
Sehemu ya rows za Server... ukibofya tu "facebooks.com" au "instagram.com" au "whatsapp.com"kwenye simu yako au kompyuta... probably taarifa hiyo inafika hapa na kisha kuaccess 'profile' yako ambayo imehifadhiwa kwenye moja ya hizi servers... na hii yote inatokea ndani ya muda mfupi kuzido hata theluthi ya sekunde
Jengo lingine jipya linajengwa hapa hapa Prineville kwa ajili ya kuhifadhi server nyingine kutokana na ukuaji wa haraka na mkubwa wa watumiaji wa mtandao huu wa kijamii


Hii ni data center ya kampuni Apple


Hii ni Data center ya kampuni ya Google  Huo ndio ulimwengu 'wao'... na huku tulipo ndio ulimwengu wetu. Wakati sisi tunahangaika kujenga viwanda vya kutengeneza panado... wenzetu wanasugua bongo namna ya kujenga "viwanda" vya kuchakata na kuhifadhi taarifa. Na huko ndiko utajiri na kushamiri kunakopatikana katika karne hii ya ishirini na moja.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog