Posts

Showing posts from June, 2019
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA SITA Waziri wa fedha Norman Lamont alikwenda moja kwa moja mpaka mahala pa kuzungumza ambako alikuwa ameandaliwa. Muda mchache uliopita alikuwa amemaliza kikao na Waziri Mkuu John Major, Waziri wa mambo ya nje Douglas Hurd, Rais wa Bodi ya Biashara nchini Uingereza Bw. Michael Heseltine na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kenneth Clarke. Alikuwa amefika hapa kutangaza uamuzi ambao ulikuwa umefikiwa na kikao hicho cha dharura. Baada ya waandishi wa habari kutulia, Waziri Lamont kwanza alianza kueleza namna ambavyo kuna hali ya dharura ya kiuchumi ambayo imeikumba Uingereza. Kwamba uchumi umeanza kwenda kombo tofauti na ambavyo walikuwa wanatarajia. Pia alieleza namna ambavyo sarafu yao ilikuwa kwenye msongo mkubwa wa kushindwa kuwezesha biashara kufanyika na kuchochea uwekezaji kutokana na kuonekana thamani yake iko juu zaidi tofauti na uhalisia. Hivyo basi kutokana na Uingereza kuwa ndan
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA TANO "…uwekezaji unahitaji subira. Ni kama vile kupaka rangi nyumba na kusubiri ikauke. Au kupanda mmea na kuusubiri ukue. Kama wewe ni mtu mwenye kupenda furaha ya haraka haraka chukua elfu kumi yako nenda 'coco beach'.!" 'Dili' ya Karne Katika sehemu iliyopita nilieleza namna ambavyo George Soros alianza kutengeneza position yenye thamani ya zaidi ya bilioni 10 za Marekani. Lakini pia tuliangalia kwa mapana maana ya 'short sell' katika soko la hisa na soko la fedha duniani. Katika sehemu hii ya tano twende taratibu hatua kwa hatua tuone namna amnavyo George Soros alishort Paundi ya Uingereza na kuifilisi benki Kuu. Karibu… Usiku wa kuamkia tarehe 16 Septemba 1992 wakati ambao ulimwengu mzima umelala George Soros kupitia Quatumn Fund alikuwa anaazima na kuuza Paundi ya Uingereza kuzidi katika kiwango kikubwa na cha kutisha. Alikuwa anaazima ku
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA NNE "…haina maana kusema kuwa unajiamini alafu unaogopa ufanya vitu hatarishi…" Nilieleza katika sehemu ya pili ya mfululizo wa makala hii kwamba, siku zote soko la dunia la fedha huwa linainfluence exchange rate ya sarafu husika. Kwa hiyo serikali ambayo imeamua kuweka fixed exchange rate mara nyingi wanajikuta wanaingia kwenye mtego wa kushiriki kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida katika soko ili kuhakikisha kwamba kiwango walichokiweka kinabakia pale pale. Lakini kuna msemo wanasema kwamba ukweli una tabia ya kutopendwa kupuuzwa. Lakini pia hata ukijenga ukuta imara kiasi gani, hauwezi kuyazuia mafuriko milele, iko siku na saa ambayo hautatarajia ukuta huo utadondoshwa na nguvu ya mafuriko. Kilichowapata Uingereza kwa kiasi fulani kilikuwa kinafanana kabisa na hiki. Mpaka kufikia mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka 1992, hali ya ndani kwa ndani serikali kulikiwa na kia
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA TATU Katika sehemu iliyopita nilieleza namna ambavyo nchi ya Uingerrza iliingia katika mpango wa ERM baada ya uchumi wao kudorora. Lakini pia nilieleza namna namna ambavyo hali ya kiuchumi ilianza kutengemaa mara tu baada ya Uingereza kuwa chini ya mpango wa ERM. Nikaeleza kwa kwa ufupi pia ni namna gani ambavyo George Soros alikuwa anaona anguko kubwa la sarafu ya Paundi tofauti na watu wengi ambavyo walikuwa wanaona kutengemaa na kushamiri kwa uchumi wa Uingereza. Kabla sijaingia ndani kueleza ni namna gani ambavyo George Soroa aliweza kutumia fursa ya dirisha ambalo aliliona katika anguko la uchumi wa Uingereza ni vyema kwanza kumuelewa hata kidogo George Soros ni nani. Tukielewa japo kwa uchache George Soros ni nani itatusaidia kuelewa saikolojia yake ya Biashara na namna ambavyo aliweza kuipigisha magoti nchi ya Uingereza mwaka 1992 na mwishoni mwa miaka ya 1990s alivyochochea anguko
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA PILI "…maisha hayajali kama uko sahihi au hauko sahihi. Bali maisha yanajengwa na kiasi gani cha faida unapata pale unapokuwa sahihi na kiasi gani cha hasara unapata pale unapokuwa hauko sahihi.." GENESIS Unapochunguza tukio lolote lile, usikimbilie kwenye hitimisho. Kwa sababu hata siku moja hakuna hitimisho linalotoa jawabu. Kila hitimisho ni muitikio akisi ya mjengeko wa chanzo au mizizi. Kwa hiyo ili kufahamu uhalisia wa suala lolote lile ni vyema kutazama matokeo yake lakini ni jambo la weledi zaidi kama ukizama na kufukua mzizi wake. Kwa hiyo kabla sijaeleza namna ambavyo George Soros aliweza kuipigisha magoti nchi nzima ya Uingereza, kisa ambacho nitakitumia kujenga hoja zangu na maoni yangu juu ya biashara ya Forex ambayo imejizolea umaarufu hivi karibuni, kwanza kabisa nataka kutumia fursa hii kufukua mzizi wa tukio la Septemba 16, 1992 ambalo kwenye sehemu ya kwanza ni
Image
BLACK WEDNESDAY: Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na Yaliyo Nyuma ya Pazia Kwa miezi kadhaa sasa tangu mara ya kwanza ambapo Mr. Ontario aandike kwa mara ya kwanza mnakasha kuhusu biashara ya Forex, nimekuwa napokea maombi kadhaa kwamba niandike japo kidogo maoni yangu au chochote kile kuhusu suala hili. Nadhani hii ni kutokana na mimi kutoonekana kwenye nyuzi zihusuzo biashara hii na kwa hiyo imefanya wasomaji wengi kutaka nitie neno japo kidogo kuhusu biashara hii. Nimekuwa nikiepuka kuandika chochote kuhusu Forex ili kuepuka kuonekana naipigia debe (kama nikiandika positively) au labda "natia mchanga kitumbua" cha watu (kama nikiandika negatively). Lakini baada ya tafakari ya kina na utafiti, nimeonelea nitie mkono kuandika yale ninayoyajua juu ya biashara hii na masuala kadhaa ambayo naamini labda watu wengi (pengine hata wale wanayoifanya) hawayajui. Hiki ninachokiandika hapa ni visa vya kweli na matukio halisi ambayo yametokea. Majina yote ni ya watu halisi i