BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA



SEHEMU YA TATU


Katika sehemu iliyopita nilieleza namna ambavyo nchi ya Uingerrza iliingia katika mpango wa ERM baada ya uchumi wao kudorora. Lakini pia nilieleza namna namna ambavyo hali ya kiuchumi ilianza kutengemaa mara tu baada ya Uingereza kuwa chini ya mpango wa ERM.
Nikaeleza kwa kwa ufupi pia ni namna gani ambavyo George Soros alikuwa anaona anguko kubwa la sarafu ya Paundi tofauti na watu wengi ambavyo walikuwa wanaona kutengemaa na kushamiri kwa uchumi wa Uingereza.
Kabla sijaingia ndani kueleza ni namna gani ambavyo George Soroa aliweza kutumia fursa ya dirisha ambalo aliliona katika anguko la uchumi wa Uingereza ni vyema kwanza kumuelewa hata kidogo George Soros ni nani. Tukielewa japo kwa uchache George Soros ni nani itatusaidia kuelewa saikolojia yake ya Biashara na namna ambavyo aliweza kuipigisha magoti nchi ya Uingereza mwaka 1992 na mwishoni mwa miaka ya 1990s alivyochochea anguko la kiuchumi la Bara zima la Asia.

GEORGE SOROS
George Soros amezaliwa mwaka 1930 (kwa sasa ana miaka 87) kwenye familia yenye asili ya Kiyahudi kwenye mji wa Budapest huko Ufalme wa Hungari kipindi hicho.
Baba yake alikuwa ni mwanasheria huku mama yake akiwa anatokea kwenye familia ambayo walikuwa wanamiliki biashara yenye mafanikio ya kuuza hariri.
Jina halisi kabisa la familia yao lilikuwa ni 'Schwartz' (alipaswa kuitwa George Schwartz) lakini kutokana na kuibuka kwa wimbi la kuchukiwa kwa Wayahudi maeneo ya Ulaya mashariki kwa kipindi hicho, ilimlazimu baba yao kubadili jina hilo la Kiyahudi na kulifanya 'Soros' kuwa jina lao la familia. Lakini pia hawakuishi kubadili jina tu, bali walikacha tamaduni na hata dini ya Kiyahudi. Jina la Soros lilikuwa linashabihiana kabisa na lugha, tamaduni na maana ya eneo la Hungari na Ulaya mashariki (Soros maana yake ni 'Mrithi').
Akiwa na miaka 13, majeshi ya Nazi ya Ujerumani yaliiweka Hungari kwenye mikono yake. Ilikuwa ni moja kati ya vioindi vigumu zaidi kwa Soros na familia yao. Kuna kipindi ilimbidi mpaka ajifanye ni muamini wa imani ya Kikristo na mtoto wa ubatizo wa Afisa wa serikali ya Hungari ili kuweza kuepuka msako wa vikosi vya Nazi ambavyo zilikuwa vinafanya msako wa nyumba kwa nyumba.

Mwaka 1947, kijana George Soros alihamia nchini Uingereza na kusoma katika chuo cha London School of Economics akiwa mwanafunzi wa Mwanafalsafa nguli wa karne ya ishirini Bw. Karl Popper. Soros alisoma kwa msaada kutoka kwenye moja ya mashirika ya jumuiya ya Quaker. Pia alisoma huku akifanya kazi mbalimbali kama vile ukuli, na uhudumu wa baa.
Baada ya kumaliza masomo hakuweza kupata kazi moja kwa moja. Kwa hiyo Soros anaeleza kwamba alitafuta anuani za benki zote zilizopo London kisha akatuma barua ya kuomba kazi kwa Wakurugenzi wote wa mabenki hayo.
Katika barua zote hizi ambazo alizituma, nyingi hazikijibiwa na wengine walimuita kwenye interview na kumdhalilisha kabisa kwa majibu mabaya na kumnyima fursa. Lakini kulikuwa na barua mbili ambazo alipata majibu mazuri. Na katika majibu hayo mawili alipewa ajira benki ya Singer & Friedlander akiwa kama afisa wa chini kabisa katika benki.
Akiwa hapa katika benki hii alitengeneza rafiki ambaye aliitwa Robert Mayer. Robert aliona ufanisi na akili ya kipekee ya George Soros katika masuala ya biashara ya fedha. Akaifikisha taarifa hii kwa baba yake ambaye alikuwa na kampuni ya 'brokage' iliyoitwa F.M Mayer ambaye ilikuwa jijini New York nchini Marekani.
Baada ya sifa hizi kumfikia baba yake, mzee Mayer mwenyewe alimuomba mwanaye amshawishi rafiki yake Soros ajiunge kwenye kampuni yake jijini New York.
Robert baada ya kumshawishi Soros kwa miezi kadhaa hatimaye akakubali na kujinga na kampuni ya brokage ya F.M Mayer huko Marekani jijini New York. Huu ulikuwa ni mwaka 1956.
George Soros alifanya kazi kwa miaka mitatu kwenye kampuni ya F.M Mayer akihuisika na masoko ya hisa ya Ulaya. Baadae mwaka 1959 alihamia kampuni ya Wertheim & Co. akiwa kama mtaalamu mchambuzi wa masoko ya hisa ya Ulaya.
Yeye mwenyewe lengo lake kuu lilikuwa ni kutunza hela ya mshahara wake kwa miaka mitano mpaka ifikie kiasi cha dola 500,000 ili aweze kurejea nchini Uingereza kuendelea na masomo yake ya Falsafa.
Ni katika kipindi hiki hiki pia ndipo ambapo alianza kukuza na kutafiti nadharia yake iitwayo "Reflexivity". Kama ambavyo nilieleza kuwa George Soros alikuwa ni mwanafunzi wa mwanafalsafa nguli Karl Popper kipindi alipokuwa anasoma London School Of Economics. Kwa hiyo hata nadharia yake hii ilikuwa na chembe chembe nyingi za kufanana na mitazamo ya Karl Popper. Katika nadharia hii kwa kifupi ni kwamba Soros anaeleza juu ya Thamani ya soko (soko la hisa na soko la fedha hasa hasa) kwamba inaendeshwa si tu na sababu za kiuchumi pekee bali pia na mitazamo na mawazo yasiyo na hakika ya washiriki katika soko. Kwamba kuna kitu anakiita 'reflexive feedback loops' ambazo zinatengenezwa kwa sababu ya mitazamo, mawazo na imani ya washiriki katka soko (traders) na mitazamo hii ndio inashawishi kutokea kwa matukio na matukio hayo nayo yanakuja kushawishi mitazamo, mawazo na imani ya washiriki wa soko kuhusu uelekeo wa soko mbeleni. Hii ndio inayofanya soko kuwa na mizunguko ambayo ni "virtuous au vicious" na hatimaye kuleta "boom au bust" kwenye soko na hivyo "kupanda au kushuka" kwa soko mahususi (au sarafu).
Nadharia hii iko tofauti sana na kile ambacho kanuni andamizi za uchumi zinavyofundisha namna ya kutambua uelekeo wa soko (au sarafu) kwa kung'amua na kuchambua equilibrium yake.
Mwaka 1963 George Soros alihamia kwenye kampuni ya Arnhold and S. Bleichroeder ambako alifanikiwa kupanda juu kwa cheo mpaka kufikia ngazi ya 'Vice President' wa kampuni. Baadae Marekani wakaanzisha utaratibu wa 'Interest Equalization Tax'. Kodi hii ilianzishwa na Rais JF Kennedy mwaka 1963 ili kupunguza kiwango cha fedha ambazo watu walikuwa wanatumia kununua dhamana (securities) za serikali za nchi za nje. Kwa wale wenye uelewa mzuri wa masuala ya uchumni na soko la fedha, tunaweza kusema kwamba serikali ya marekani walianzisha mpango huu ili kupunguza 'balance-of-payment' deficit.
Kwa kuwa Soros alikuwa anahusika hasa na soko la Ulaya mpango huu wa serikali ulimuathiri sana.
Hiki ni moja ya kipindi ambacho morali ya Soros juu ya soko la fedha ilishuka kwa kiwango kikumbwa sana. Alitumia muda wake mwingi kutoka 1963 mpaka 1966 kuandika dessertation yake ya Falsafa.
Lakini kwa bahati nzuri akiwa anaendelea kuandika dessertation, aliwiwa tena na kutamani kuanza kufanyia majaribio nadharia yake ya 'reflexivity'. Akatenga kiasi cha dola 100,000 na kuanza kufanya majaribio ya 'kutrade' kwa kutumia strategy ambazo aliziunda kutoka kwenye nadharia yake ya 'reflexivity'.
Mafanikio yalikuwa ni makubwa na ya kuridhisha.
Mwaka 1969 aliamua kuanzisha kampuni ya Double Eagle Hedge Fund ambapo yeye mwenyewe aliwekeza kiasi cha dola 250,000 na alipata wawekezaji waliowekeza jumla ka dola milioni 4.
Ndani ya mwaka mmoja mtaji ule wa dola milioni 4 ulikuwa mpaka kuwa dola milioni 12. Ndipo hapa ambapo Soros aliona fursa ya kuanzisha kitu kikubwa zaidi.
Mwaka uliofuata yaani 1970, George Soros kwa kushirikiana na Jim Rogers walianzisha Quatum Fund (mwanzoni ilisajiliwa kama Soros Fund Management).
Sasa hii Quatum Fund ndio 'muwa' uliozamisha meli ya Uingereza.. na si Uingereza tu, bali pia ndio muwa uliozamisha meli ya nchi za Asia mwishoni mwa miaka ya tisini.


George Soros na Barack Obama

Nimeeleza hapo juu kwamba ili tuelewe saikolojia ya biashara ya George Soros ni vyema kwanza tumuelewe Soros na alikotoka. Lakini pia kabla ya kuangalia tukio la 1992 namna ambavyo alizamisha Benki Kuu ya Uingereza… ni vyema kwanza kuelewa Kampuni ya George Soros, Quatum Fund inafanya nini hasa?
Kwanza kabisa jambo la kwanza kulielewa kabla ya yote, Quatum Fund sio 'brokage firm' kama ambavyo kampuni zote huko nyuma ambazo Soros alikuwa ameajiriwa nazo.
Quatum Fund ni moja ya aina za kumpuni ambazo zinajulikana kwa jina maarufu la 'hedge funds'. Inawezekana George Soros ni moja ya watu waliochangia kwa kiasi kikubwa kujulikana kwa jina hili la 'hedge funds' lakini pia hakuna ubishi kwamba George Soros ndiye hedge fund manager aliyefanikiwa zaidi duniani tangu kuibuka kwa sekta hii.
Hedge funds ni kitu gani hasa??
Kwa tafsiri rahisi na fupi, hedge funds ni makampuni makubwa ya fedha ambayo biashara yake wanafanya kwa kuwekeza kiwango kikubwa cha pesa kwa kwenye biashara za hela zenye risk kubwa au namna fulani ya 'kubet' kwamba tukio fulani litatokea na hivyo kuwapatia faida. Pia makampuni haya wanatumia namna nyingine za 'financial instruments' ili kuhakikisha kwamba hawapati hasara kwenye hizi risk au 'bet' wanazofanya.
Lets do this… twende taratibu!
Tuseme kwa mfano TMT ya Ontario tuichukulie kwamba ni hedge fund (mfano tu). Katika kufanya uchambuzi wao, au wakapata taarifa fulani kwamba kuna tukio fulani kubwa litatokea ndani ya wiki chache zijazo na kusababisha anguko kubwa la thamani ya hisa za kampuni ya Vodacom zitaporomoka thamani yake kwa kiwango kikubwa sana. Kwa hiyo TMT wanaweza kubet against it.
Unafanyaje?
TMT wanaweza 'ku-short' hisa za Airtel, kwa maana ya kwamba watatengeneza faida kama kweli ikitokea hisa za Airtel zikaporomoka kweli.
Lakini ikumbukwe ukweli ni kwamba sekta ya mawasiliano inakua kwa kasi, kwa hiyo licha ya wao kuhisi kwamba kuna tukio litatokea na kusababisha anguko la hisa za kampuni ya Airtel kuporomoka , lakini pia kuna uwezekano fulani wa hisa hizo kupanda thamani.
Kwa hiyo unachofanya unanunua pia hisa za kumpuni ya TTCL pia (Airtel wanamiliki TTCL) . Hii inasaidia kujiweka kwenye sehemu nzuri kama ikitokea hisa za makampuni ya Airtel zikipanda. Ndio hapa tunasema unahedge.
Ikumbukwe pia kwamba uwekezaji huu unaofanywa na TMT (hedge fund) ni wa mabilioni ya pesa.
Sasa basi ikitokea kwamba anguko la thamani ya hisa za Airtel halijatokea na badala yake zikapanda na TTCL nayo zikipanda kwa kuwa kampuni hizo zinahusiana… alafu thamani ya hisa za TTCL zikipanda kwa kasi kuliko zile za Airtel, maana yake ni kwamba TMT watapata faida. Na pia ikitokea tukio walilodhani likatokea na hisa za thamani ya Airtel ikaporomoka… maana yake ni kwamba TMT watapata pia faida.
Hii ndio maana ya 'hedging'. Namna fulani ya ku-take risk alafu unatengeneza mazingira ya kupata usalama ndani ya hiyo risk.
Kuna swali moja ambalo naamini watu wengi watakuwa wanajiuliza muda huu… "unatengenezaje fedha ikitokea umenunua hisa za kampuni na kisha zikaporomoka thamani?".
Katika pekua pekua zangu nimegundua hata baadhi ya wanafunzi wa Mr. Ontario huwa wanauliza swali hili… kwamba inakuwaje 'ukisell' currency ikiwa juu alafu ikishuka ndio upate faida? Inaonekana kama vice vesa!!
Tukifikia hatua ya kujadili trade aliyoifanya Soros na kuifilisi benki kuu ya Uingereza, kwa faida ya wengi nitagusia namna 'short sell' inavyotokea na kwa nini unapata faida pale thamani ya sarafu husika au hisa za kampuni husika zikishuka.
Kwa sasa naamini tumepata picha walau kidogo namna ambavyo hedge funds zinavyofanya kazi. Jambo lingine la msingi zaidi kulijua ni kwamba… ikitokea kampuni hizi wakiwa na uhakika mkubwa wa kutokea kwa tukio fulani na kujua namna ambavyo thamanibya hisa au sarafu zitakavyoporomoka… wanakopa mabilioni kwa mabilioni ya fedha na kuwekeza kwenye 'trade' husika.
Kwa mfano nilioutoa hapo juu, kama TMT wakiwekeza hela zao kwenye trade ya hapo juu kwa kushort sell hisa za Vodacom na kweli zikaporomoka, maana yake ni kwamba watatengeneza faida ya wastani. Lakini vuta picha kama fedha yote watakayowekeza kwenye hiyo short sell ni fedha za benki fulani. Maana yake faida itakuwa ni maradufu.
Jambo lingine la msingi la kulifahamu kuhusu hedge funds ni namna gani wanapata fedha zao. Kampuni yoyote ya hedge funds wale Managers (Mfano kama alivyo George Soros kwa Quatum Fund) hawawekezi fedha zao. Bali ni fedha za watu matajiri na mifuko au mashirika ya fedha.
Katika fedha hizi ambazo matajiri na mashirika ya fedha wanawekeza kwenye hedge fund kwa viwango standard, 2% inatolewa kwa ajili ya Manager (s). Hii haijalishi kama kuna faida inatengenezwa au la, lakini kila mwaka 2% inatolewa kwa ajili ya Manager (waanzilishi wa hiyo hedge fund).
Na pia 20% faida inayopatikana kwenye kila trade inakwenda kwa Managers. Mfano kama hapo juu huo mfano wa TMT kushort sell hisa za Vodacom, kama hiyo trade kwa mfano ingetemgeneza kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni 20 kwa mfano. Maana yake Bwana Ontario ataenda kulala na shilingi Bilioni 4 kibindoni.

Kwa hiyo nikiongelea George Soros na kampuni yake ya Quatumn Fund hiki ndicho ninachomaanisha.

Turudi kwenye tukio la Soros kuifilisi Benki Kuu…
Nilieleza kwamba Uingereza na Waziri mkuu John Mayor walikuwa wanashangilia uchumi kutengemaa. Lakini Soros alikuwa haoni kutengemaa kiuchumi.. aliona kitu kingine kabisa.
Ni nini?
Aliona 'a miss priced currency'. Uingereza ilipoingia kwenye mpango wa ERM Puandi ya Uingereza ilipewa thamani kati ya 2.78 mpaka 3.13 ya DM ya Ujerumani.
Soros aliona viashiria kadhaa kuamini kwamba hii haikuwa thamani ya Paundi ya Uingereza. Aliamini bila shaka yoyote nafsini mwake kwamba Paundi ya Uingereza ilikuwa na thamani chini ya hapa kwa kiwango kikubwa sana. Kwamba Paundi ya Uingereza imepewa thamani kubwa kupindukia tofauti na uhalisia ambao yeye aliona ni sahihi.
Kitu pekee ambacho alikuwa anahitaji, ni misuli ya mtaji wa fedha ya kutosha aweze kuitingisha nchi ya Uingereza.

Itaendelea…

Comments

Popular posts from this blog