BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA

SEHEMU YA NNE

"…haina maana kusema kuwa unajiamini alafu unaogopa ufanya vitu hatarishi…"


Nilieleza katika sehemu ya pili ya mfululizo wa makala hii kwamba, siku zote soko la dunia la fedha huwa linainfluence exchange rate ya sarafu husika. Kwa hiyo serikali ambayo imeamua kuweka fixed exchange rate mara nyingi wanajikuta wanaingia kwenye mtego wa kushiriki kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida katika soko ili kuhakikisha kwamba kiwango walichokiweka kinabakia pale pale.
Lakini kuna msemo wanasema kwamba ukweli una tabia ya kutopendwa kupuuzwa. Lakini pia hata ukijenga ukuta imara kiasi gani, hauwezi kuyazuia mafuriko milele, iko siku na saa ambayo hautatarajia ukuta huo utadondoshwa na nguvu ya mafuriko.
Kilichowapata Uingereza kwa kiasi fulani kilikuwa kinafanana kabisa na hiki.

Mpaka kufikia mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka 1992, hali ya ndani kwa ndani serikali kulikiwa na kiasi kikubwa cha taharuki juu ya uhalisia wa thamani ya Paundi.
Japokuwa viongozi wa serikali katika vikao vyao na waandishi wa habari na Bungeni walikuwa wanajitahidi kuonyesha nyuso za furaha lakini uhalisia ni kwamba taharuki ilikuwa ni kubwa mno chini kwa chini hasa hasa kwa Exchequer (Hazina ya Uingereza).
Kulikuwa hakuna ubishi kwamba thamani ya Paundi ambayo ilipewa baada ya kujiunga na mpango wa ERM haikuwa sahihi. Paundi ilipewa thamani kubwa sana tofauti na uhalisia.
Licha ya taharuki kubwa ambayo ilikuwa inafukuta ndani kwa ndani, maswali yalipokuwa yakiulizwa na vyombo vya habari… serikali ilikuwa inajiapiza kuwa watahakikisha thamani ya Paundi inabaki juu na hivyo wanaoinunua kwenye soko la kimataifa wasiwe na shaka yoyote.
Uchumi ukaendelea kuonekama unashamiri na soko la fedha likaendelea 'kutrade' Paundi ya Uingereza katika kiwango cha kuridhisha kabisa.
Lakini uhalisia fukuto la chini kwa chini lilikuwa ni kubwa kweli kweli.
Kwanza kabisa Puaundi ilikuwa inatrade katika 'lower end', kwa kiwango cha mwisho kabisa ambacho kilikuwa kimeruhusiwa chini ya mpango wa ERM (2.78 DM). Maana yake ni kwamba presha ya kushuka chini kwa thamani ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba ilikuwa inailazimu serikali kuweka kiwango hicho cha mwisho kabisa ili kukidhi masharti ya mpango wa ERM.
Lakini Pili, nchi ya Uingereza ilikuwa na 'current account deficit' kubwa kupita kawaida. Maana yake ni kwamba licha ya dalili za kutengemaa kwa uchumi lakini walikuwa wananunua na kuagiza zaidi bidhaa kutoka nje kuzidi vile ambavyo walikuwa wanauza.
Hizi zote zilikuwa ni dalili za wazi kwamba kuna tatizo kubwa linalofukuta chini kwa chini katika uchumi wa Uingereza na serikali walikuwa wanatumia mabavu ya mpango wa ERM kuendelea kuweka juu thamani ya Paundi.
Huko nje serikali ilikuwa inaendelea kujitutumua kuwa thamani ya Paundi itabaki pale ilipo.
Watu wa masoko ya fedha waliendelea kuamini kauli hii ya serikali na biashara zikaendelea kama kawaida. Kujitutumua huku kwa serikali ya Uingereza kuliwawezesha kuvuka robo ya kwanza na robo ya pili ya mwaka na hatimaye kuingia robo ya tatu.
George Soros kutokana na kubobea kwenye uchambuzi na kufuatilia masoko ya hisa na masoko ya fedha kwa miaka kadhaa, naamini alilikuwa mtu wa kwanza kabisa nje ya serikali ya Uingereza kung'amua hili mapema, kwamba kulikuwa na hatari ya anguko kubwa la kiuchumi kutokea.

George Soros miaka ya tisini


Mara tu baada ya George Soros kuhisi 'harufu' ya tukio kubwa la kiuchumi kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kwenda kutokea akaanza 'kukunja misuli' yake vyema ya kiutendaji.
Nilieleza kwamba hedge funds mara nyingi (na kwa uhalisia ni mara zote) wanajihusisha na biashara za fedha zenye hatari kubwa ya hasara au faida. Na mara nyingi hizi 'scheme' ambazo huwa wanazifanya huwa zinalenga uwezekano wa kutokea matukio fulani makubwa ambayo yataathiri nguvu ya sarafu au uchumi wa nchi husika au hisa za kampuni fulani wanayoilenga.
Kwa hiyo hii 'harufu' ambayo George Soros aliinusa ilikuwa ni fursa adhimu kwake na kampuni yake ya Quatumn Fund kutokana na asili ya biashara zao sekta ya hedge funds.
Kwa hiyo mwanzoni kabisa mwa mwezi August 1992, Gorge Soros akaanza kutengeneza 'position' yenye thamani ya dola bilioni 1.5 ( Karibia Trilioni 4 za Kitanzania). Wengi waliopita pale darasani TMT kwa Bw. Ontario (au mahala kwingine) naamini wanaweza kuelewa nikisema 'kutengeneza Position', lakini kwa faida ya wote, Position ni kile kitendo cha trader kuweka 'commitment' ya kuuza au kununua kiasi fulani cha financial instrumet (hisa, sarafu, dhamani za serikali au hati fungani) kwa gharama mahususi.
Kwa hiyo taratibu hapo mwanzoni mwa mwezi August 1992, Soros akaanza kutengeneza hiyo position ya dola bilioni 1.5 ambapo position hiyo ilikuwa ni 'short sell'.
Kiti pekee ambacho alikuwa anakisubiri ni kupata 'good entry point' aweze kuingia miguu yote miwili katika position hiyo. Na hiyo entry point ambayo alikuwa anaisubiria ilikuwa ni kiashiria cha kuanza kuanguka rasmi kwa Paundi kwenye soko la dunia.
Serikali ya Uingereza iliendelea kutunisha misuli. Thamani ya Paundi ikaendelea kuwekwa juu kuzidi
uhalisia. Wafanyabiashara wengi kwenye soko la fedha la dunia waliendelea kuwa na imani juu ya Paundi lakini George Soros bado aliendelea kuwa na ndoto kwamba lazima Paundi idondoke.
Joto na fukuto la ndani kwa ndani likapanda kweli kweli. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi wa nane joto hili likaanza kuvuka nje ya mipaka ya Uingereza. Watu wa ndani wa mabenki kuu mengine, hasa hasa benki ya 'Buba' (Bundesbank - Benki Kuu ya Ujerumani) ambayo ndiyo ilikuwa na ushawishi mkubwa zaidi kwenye soko la fedha ulaya wakaanza minong'ono ya kwamba Paundi ilikuwa imewekwa thamani ya juu mno kuzidi uhalisia. Hii ilikuwa inazorotesha biashara kati ya Uingereza na nchi nyingine, na pia kufanya uchumi wa Uingereza udorore na mtokeo yake kuwagharimu nchi nyingine zote za Ulaya.
Kwa mfano, siku ya August 25 moja ya wajumbe wa bodi ya Bundesbank, Bw. Reimut Jochumsen alitoa hutuba ambayo ilieleza uwezekano wa kufanya marekebisho baadhi ya sarafu.
Baadae pia wiki hiyi kuna afisa wa Bundesbank ambaye hakutajwa jina na vyombo vya habari ambaye alitoa maneno ya kuonyesha kutoridhishwa na thamani ya Paundi ilivyowekwa.
Yote haya yalizidi kuweka presha kwenye thamani ya Paundi kwenye soko. Na imani ya Soros kwamba Paundi inaelekea kuporomoka ilizidi kuimarika.
Mwezi wa August hatimaye ukapita kwa salama huku serikali ya Uingereza ikiendelea kutunisha msuli na thamani ya Paundi ilibaki pale pale.
Lakini gharika lilikuja katikati ya mwezi Septemba… presha ilikuwa kubwa zaidi. Uchumi wa Uingereza ulizidi kuzorota, current account deficit ilikuwa kubwa zaidi na watu wa ndani wa mabenki makuu mengine ya Ulaya uvumilivu wao ukaanza kukoma.
Rais wa Benki kuu ya Ujerumani, Bundesbank, Profesa Helmut Schlesinger alifanya mahojiano na Wall Street Journal. Katika mahojiano hayo waliongea masuala mengi yahusuyo hali ya kiuchumi ya Ulaya na masuala mengine mengi ya kibenki.
Katika mahojiano hayo ambayo yalichapwa kwenye ukurasa mzima wa jarida la WallStree Journal kulikuwa na kitu kidogo sana, aya moja tu ambayo kwa haraka haraka ilionekana ni ya kawaida lakini ndiyo hasa George Soros alipoiona ilimpatia 'good entry point' na hatimaye ilipelekea anguko la benki kuu ya Uingereza.
Jarida hili baada ya kutua mezani kwa Soros, alipoisoma mahojiano hayo na Rais wa Benki Kuu ya Ujerumani… katika ukurasa mzima wa hayo mahojiani kuna paraghaph moja tu ambapo alipoisoma moyo ulimlipuka.
Nanukuu kama ambavyo iliandikwa na Wall Street Journal;
"…the president of the Bundesbank, Professor Helmut Schlesinger, does not rule out the possibility that, even after the realignment and the cut in German Interest Rates, one or two currencies could come under pressure before the referendum in France. He conceded in an interview that the problem are of course not solved completely by the measures taken…"
Aya hii moja tu kwenye interview yote iliyopamba ukurasa mzima wa jarida, ndiyo ambayo ilizua kizaa chote. Ni aya hii ambayo Soros aliitumia kuthibitisha imani yake ambayo alikuwa nayo kwa miezi kadhaa kwamba Paundi ya Uingereza ilikiwa inaelekea kudondoka kwa kishindo.
Nimeanza sehemu hii ya nne kwa maneno haya kwa makusudi kabisa, kwamba "…haina maana kusema kuwa unajiamini alafu unaogopa ufanya vitu hatarishi…"
George Soros japokuwa alikuwa anafanya kitu cha hatari sana, lakini imani yake kuhusu tukio la kuanguka kwa Paundi ilikuwa ni kubwa na sasa ilithibitika zaidi. Hivyo alikata shauri, "…haina maana kusema kuwa unajiamini alafu unaogopa ufanya vitu hatarishi…"
Akaongeza mtaji kwa kuazima mabilioni ya dola na kuongeza position yake kutoka dola bilioni 1.5 mpaka dola bilioni 10 (zaidi ya trilioni 22 za kitanzania).
(Baadae Soros aliongeza tena hii position… nitaeleza)

Sasa kabla sijaenda mbali zaidi naomba kama nilivyoahidi kwenye sehemu iliyopita nieleze namna ambavyo "short-sell" inavyokuwa na kwa nini unapata faida thamani ya hiyo sarafu (au hisa) inaposhuka.
Tuanze kwa mfano rahisi…
Tutumie mfano ule ule wa hisa za kampuni ya Airtel.
Tuseme kwamba hedge fund fulani wamefanya uchambuzi na kuhisi kwamba hisa za kampuni ya Airtel zimefika kilele cha juu kabisa ya thamani yake na kuna tukio litatokea na litasababisha anguko kubwa la hisa hizo. Tuseme kwamba kwa sasa kila hisa moja ya Airtel ina thamani ya Tshs. 5,000/- na unahisi kwa hakika kabisa kuwa kuna anguko litatokea na thamani ya hisa hizi kushuka.
Kwa hiyo unachokifanya unashort sell.
Inakuwaje?
Unaenda kwa broker, au mtu au kampuni ambayo wanamiliki kiwango fulani kikubwa cha hisa za Airtel na kuazima kiasi fulani cha hisa hizo.
Kwa mfano tuseme TMT ya Ontario wanamiliki kiwango kikubwa cha hisa za Airtel, kwa hiyo unaenda na kuazima kwao labda tuseme hisa milioni moja. Naomba nieleweke hapa, haununui hisa hizo, unaziazima kama hisa.
TMT watakupa masharti labda uzirudishe hisa hizo ndani ya miezi mitatu labda mathalani, na ukizirudisha utarudisha na riba ya 10% ya thamani ya hisa hizo.

Profesa Helmut Schlesinger (kulia mwenye miwani) aliyekuwa Rais wa 'Buba' (Bundesbank - Benki Kuu ya Ujerumani)



Kwa hiyo baada ya miezi mitatu, utawarudisia TMT hisa milioni moja (ikumbukwe sio fedha shilingi milioni moja bali ni hisa milioni moja) pia utawapa na fedha za riba 10% ya thamani ya hisa walizokupa. Maana yake utawapa fedha shilingi milioni 500 na hisa zao milioni moja.
Katika ile miezi mitatu wewe unanufaikaje?
Nilieleza kwamba unafanya short sell pale pekee ukihisi kuna uwezekano mkubwa wa anguko la hisa au sarafu fulani.
Kwa hiyo baada ya kuchukua hisa hizo milioni moja kutoka TMT (ambazo thamani yake ni shilingi bilioni tano na nasisitiza tena hauzinunui bali unaziazima kama hisa na unazirudisha kama hisa) unaanza kuziuza sokoni.
Kwa hiyo kwa kuwa hisa hizo zina thamani ya 5,000/- kila hisa, maana yake ukiuza hisa hizo milioni moja utapata jumla ya shilingi bilioni tano.
Kama uko sahihi na lile tukio ambalo umelihisi na likatokea kweli na hisa za Airtel zikaporomoka kweli, mfano ndani ya miezi hiyo mitatu kutoka ile 5,000/- mpaka kufikia 1,000/- kwa hisa moja.
Unachofanya baada ya miezi mitatu hiyo unaenda kwenye soko la hisa na kuzinunua tena hisa milioni moja kwa thamani ya 1,000/- ya thamani ya sasa kwa kila hisa.
Maana yake ni kwamba miezi mitatu iliyopita uliazima hisa milioni moja ukaziuza kwa thamani ya shilingi 5,000/- na kupata shilingi bilioni 5. Kwa hiyo leo hii ukizinunua tena kwenye soko la hisa (baada ya tukio kutokea na thamani kuporomoka) maana yake utazinunua kwa jumla ya bilioni 1 tu.
Kwa hiyo unakuwa umetengeneza faida ya bilioni 4. Ukitoa ile 10% riba ya TMT (milioni 500) unabakiwa na faida ya shilingi 3.5 Bilioni za kitanzania.
Hiyo ndivyo short sell inavyofanyika.
Je short sell ya sarafu inakuwaje?
Tuseme kwa mfano unataka kushort sell 'Tshs' na leo hii dola moja ya marekani ina thamani ya shilingi 2,000 ya Tanzania. Kwa hiyo unaenda kwenye bank, au kampuni au mtu binafsi na kuazima kiasi kikubwa cha shilingi. Labda tuseme shilingi bilioni 5.
Lengo lako ni kushort sell 'Tsh' kwa kuwa umeona kuna tukio fulani litatokea na kusababisha thamani ya shilingi kuporomoka.
Kwa hiyo tuseme ukaingia mkataba na Mzee Kimei na CRDB yake na wakakupa hizo shilingi bilioni 5. Lakini wakataka urudishe na riba ya 5% (shilingi milioni 250).
Ikumbukwe kwamba wewe unafahamu kwa mujibu wa chambuzi zako kwamba thamani ya shilingi inaelekea kuporomoka. Kwa hiyo 'unachenji' zile shilingi bilioni 5 za kitanzania kuwa dola 2.5 Milioni.
Baada ya mwezi mmoja tukio ulilolihisi likatokea na thamani ya shilingi kuporomoka kutoka shilingi 2,000 kwa dola moja na kuwa 3,500 kwa dola moja.
Kwa hiyo hapa unabadili tena hizi dola milioni 2.5 kuwa shilingi na utapata jumla ya shilingi bilioni 8.75.
Utarudisha shilingi bilioni 5 ya Mzee Kimea na CRBD yake pamoja na riba yao ya 5%, na mfukoni utabakiwa na shilingi bilioni 3.5.!
My friends… hiyo ndiyo short sell na hivyo ndivyo ambavyo watu wanatajirika katila global financial markets.

Nieleze sasa short sell ya George Soros na namna alivyoifilisi benki kuu ya Uingereza.

Stay tuned…

Comments

Popular posts from this blog