BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA

SEHEMU YA SITA

Waziri wa fedha Norman Lamont alikwenda moja kwa moja mpaka mahala pa kuzungumza ambako alikuwa ameandaliwa.
Muda mchache uliopita alikuwa amemaliza kikao na Waziri Mkuu John Major, Waziri wa mambo ya nje Douglas Hurd, Rais wa Bodi ya Biashara nchini Uingereza Bw. Michael Heseltine na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kenneth Clarke. Alikuwa amefika hapa kutangaza uamuzi ambao ulikuwa umefikiwa na kikao hicho cha dharura.
Baada ya waandishi wa habari kutulia, Waziri Lamont kwanza alianza kueleza namna ambavyo kuna hali ya dharura ya kiuchumi ambayo imeikumba Uingereza. Kwamba uchumi umeanza kwenda kombo tofauti na ambavyo walikuwa wanatarajia. Pia alieleza namna ambavyo sarafu yao ilikuwa kwenye msongo mkubwa wa kushindwa kuwezesha biashara kufanyika na kuchochea uwekezaji kutokana na kuonekana thamani yake iko juu zaidi tofauti na uhalisia.
Hivyo basi kutokana na Uingereza kuwa ndani ya mpango wa ERM ambao unatoa sharti la kuweka thamani ya Paundi kati ya 2.78 DM na 3.31 DM, kwa hiyo kwa masikitiko makubwa Waziri Lamont alitangaza kwamba Uingereza inajitoa kwenye mpango wa ERM na kufloat sarafu yake (kuacha thamani ya sarafu iamuliwe na soko la fedha).
Waziri Lamont alieleza pia kuwa interest rates inashushwa mpaka 12% (kesho yake ilishushwa tena kurudi 10%).
Kimya cha woga kilitawala kwenye chumba cha mkutano wa habari, lakini huko jijini New York kwenye ofisi za Quatumn Fund pamoja na ofisi nyingine zote za hedge funds na wafanyabiashara wa fedha kulitawaliwa na vifijo na nderemo.
George Soros na wote walioamini katika kile ambacho alikuwa anakiona kwa muda wa miezi miwili iliyopita walikuwa wameshinda ushindi wa kishindo.
Dakika chache tu baada ya Waziri Lamont kutangaza kuwa Uingereza wanajitoa kwenye mpango wa ERM na kufloat sarafu yao, thamani ya Paundi ilishuka kwa 25% dhidi ya dola.
Nilieleza kwamba position ya Soros dhidi ya Paundi ilikuwa na thamani ya $ 15 Bilioni. Siku hiyo mara tu baada ya Waziri Lamont kutoa tangazo la kufloat Paundi, thamani ya position ya Soros ilipanda mpaka $ 19 Bilioni na wiki mbili baadae ikaongezeka mpaka $ 22 Bilioni. Au kwa maneno machache, George Soros na Quatumn Fund walitengeneza faida ya Dolla Bilioni saba.!!
Nilieleza kuwa Hedge Fund managers wanapata 20% ya kila trade ambayo inaleta faida kwenye kampuni. Kwa hiyo katika trade George Soros alipata kiasi cha dollar billion 1.4 za kimarekani.
Asili ya biashara ya fedha ni kwamba kama wewe ukipata faida maana yake kwamba kuna mtu anapata hasara. Na katika trade hii George Soros alipata faida hiyo ya kutisha huku Benki kuu ya Uingereza ikiingia kwenye hasara ya karibia Dollar Billion 10 za kimarekani. Pamoja na hasara hii pia Uingereza walikuwa wamepoteza mabilioni ya akiba ya fedha za kigeni siku hiyo walipokuwa wakijitahidi kuokoa thamani ya Paundi.
Mwanzoni kabisa mwa makala hii nilieleza kwamba kabla ya mwaka 1992 kipindi Margareth Thatcher alipokuwa Waziri Mkuu, alipinga vikali Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM na serikali kujihusisha kwenye kuweka exchange rate ya Paundi. Alitala thamani ya Paundi iamukiwe na soko. Lakini John Major na wafuasi wake walipambana vikali kutaka Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM.
Kwa kuwa kipindi kile Uingereza ilikuwa kwenye mdororo mkali wa Kiuchumi hakuna mtu ambaye alimsikiliza Margareth Thatcher.
Hatimaye John Major aliingia madarakani huku akitumia mpango wa ERM kama mtaji wake kisiasa. Kwa hiyo kitendo cha kutokea anguko kubwa hivi la thamani ya Puandi kushuka na Uingereza kujitoa kwenye mpango wa ERM kulimgharibu mno. Hakuwa tena na mtaji wa kisiasa na wananchi wa Uingereza walimuona kama yeye ndiye ambaye aliwatumbukiza kwenye shimo hilo. Kwa hiyo kwenye uchaguzi uliofuata John Major na chama chake waliondolewa madarakani.
Na siku hii ya 16 September 1992 ni siku ambayo watu wa Uingereza hawaisahau maisha yao yote kutokana na machungu ambayo waliyapata na ndipo hapa waliibatiza jina kwamba ni BLACK WEDNESDAY.!
Lakini siku hii ndiyo siku ambayo Soros aliandika jina lake kwenye historia ya Dunia na kujizolea umaarufu kwenye soko la fedha la dunia na kudhihirisha kwamba yeye ni moja ya traders bora zaidi wa soko la fedha kuwahi kutokea chini ya jua.

Chiefs, hiyo ndiyo nguvu ya biashara ya Forex. Trader mmoja tu, tena ambaye kipindi hicho hakuwa na umaarufu au ushawishi mkubwa… lakini alitunishiana misuli ya kibiashara na maarifa ya soko la fedha dhidi ya benki kuu ya nchi na nchi nzima na kuwashinda na kutengeneza utajiri ndani ya siku moja tu.

Mpaka hapa nimeongelea upande mmoja wa biashara ya Forex (Nguvu ya Biashara hiyo) bado upande wa pili (yaliyo nyuma ya pazia) ambapo inahusu 'market markers' namna wanavyofanya kazi na kuathiri soko la fedha na namna ya kukabiliana nao.
Kipengele hicho nitakuwa naweka taratibu taratibu kama vidokezo (kwenye Morning and Evening Bulletins) ila mpaka hapa niseme kamba Makala hii imefika mwisho.
Naamini kwamba kuna kitu umepata na kujifunza.
My Personal Expirience with Forex
Binafsi mara yangu ya kwanza kusikia hili suala ilikuwa ni mwaka 2013. Nimewahi kufanya kazi 'maalumu' na Shirika la World Vision Tanzania hasa kwenye programu zao vijana. Kuna siku nilikuwa naandaa 'speech' kuna vijana wa sekondari nilialikwa kuzungumza nao. Nikiwa kwenye maandalizi hayo ya speech nikawa natafuta mfano mzuri wa kijana mdogo ambaye amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwenye sekta aliyopo, nikawa naperuzi mtandaoni kuona kama naweza kupata mifano mizuri, ndipo nikakutana na Makala kuhusu kijana Sandile Shezi wa Afrika Kusini ambaye nadhani ni moja ya watu waliofanikiwa zaidi barani Afrika kwenye biashara ya Forex. Kipindi kile naisoma ile makala alikuwa na kama miaka 21 tu au 22.
Nilivutiwa sana na stori yake. Kwa hiyo hata baada ya kuandika speech yangu na kuzungumza na wale wanafunzi niliendelea kumfuatilia Sandile na mambo ambayo alikuwa anayafanya.
Kwa hiyo kwa kipindi kirefu nilikuwa najua kuhusu forex na inahusu nini lakini sikudhani kama inawezekana kuifanya ukiwa Tanzania. Kwamba hakuna infrastructure ya kuwezesha mtu kufanya forex ukiwa Tanzania. Kwa hiyo nikawa nafuatilia tu wafanyabiashara ya Forex (hasa Sandile) kama hobby.
Mwaka jana 2017, Ontario akaandika makala kuhusu biashara hii na ndiye alinifumbua macho kwamba inawezekana kabisa kuifanya hata hapa Tanzania kwa urahisi. Kwa hiyo nilifutilia kwa karibu sana kile ambacho kilikuwa kinaendelea.
Baadae tukawasiliana na akanieleza ni namna gani itafanyika na kadhalika na kadhalika. Akanipatia na vitabu ambavyo yeye amevisoma ushauri mwingine mwingi tu.
Hatimaye mwezi October nikahisi kwamba niko tayari kuanza biashara hiyo, kwa hiyo nikajiandikisha pale ofisini kwake ili kupata mafunzo rasmi na kisha kuanza kutrade.
Kwa hiyo nikahudhuria mafunzo, nikamaliza, nikaingia sokoni.
Kwa kuwa mimi na yeye wote ni vijana wenye ndoto kubwa, huwa tunakutana mara kadhaa na huyu jamaa kujadili masuala kadha wa kadha nje ya Forex. Baada ya kumaliza yale mafunzo, tukionana nilikuwa namwambia kuwa nataka kuwa 'best forex trader' kwenye hii nchi. Naye akawa anadai kuwa nitakuwa best ila sio juu yake (yani labda niwe namba mbili). Basi tunacheka tunaendelea na mijadala mingine.
Lakini binafsi nilikuwa namaanisha kabisa kwamba nataka niwe 'kipanga' wa Forex.
Nikaanza kutrade. Nikaweka hela kidogo tu kwanza kupima upepo. Nikaweka dola 320.
Wiki ya kwanza ya kutrade nili double akaunti yangu. Wiki ya pili akaunti yangu ikakua mpaka kufikia dola 1600 na ushee. Nikapata kale kaugonjwa ambao wote kwenye forex wanakapata. Ukianza kupata faida tu unajihisi umekuwa Guru. Nilijihisi Guru kweli kweli na naelekea kweli kuwa best trader.
Nikaanza strategy za hatari hatari, kuna kitu kinaitwa Scalping. Nikaanza kufanya hiyo. Hii ni skill ambayo watu inawachukua miaka kuidevelop, lakini mimi wiki mbili nikajihisi nina mabavu ya kuscalp.
Wiki ya tatu akaunti yangu ya Forex ya dola 1600 na ushei ilishuka mpaka ikawa inasoma chini ya sifuri (negative). Kwenye forex wanasema nikaunguza akaunti.
Inauma. Inatia hasira. Inachukiza.
Lakini nikajifunza kitu. Kitu kikubwa sana. Kwamba forex is not a game… maana ilifika kipindi nilikuwa natrade kama vile nacheza gemu la nyoka. Nilijiamini kupitiliza.
Nikajifunza kwamba ni biashara ambayo inahitaji kutulia. Inahitaji kutafakari maamuzi yako. Inahitaji strategy. Inahitaji kujifunza kila siku.
Nikajifunza pia kutumia moja ya turufu yangu kuu ambayo Mwenyezi Mungu amenibariki… Utulivu wa ndani.
Nikapumzika kama wiki mbili hivi… nilitoka mpaka kwenye group zote za Forex. Walioko huko wanafahamu japo hawakuelewa kwa nini nilitoka. Baada ya wiki mbili nikarejea. Nikiwa na utulivu huku nikiapproach soko na strategies. Kwa utulivu na targets za nini ambacho nakitaka… sio sifa tu kuwa 'best trader'.
Na tangu nirejee alhamdullilah… nafanya vizuri kwenye soko kuzidi mara ya kwanza. Sipendi kuongelea ni kiwango gani natengeneza but ni kiwango cha kuridhisha kabisa. Natamani niweke screenshot hapa za moja ya trade yangu lakini sitaki kuonekana kwamba najikweza au kutafuta sifa au vinginevyo. But ukilipatia na kulielewa soko unaweza kutengeneza mishahara ya watu kadhaa ndani ya masaa machache tu.
Niseme tu alhamdulliah walau sasa naona uhalisia wa kumtimizia Cheupe wangu ndoto yake ya muda mrefu… BMW X6. Soon. Inshallah.!!



Hii risiti nilivyofund account mara ya kwanza




FNB Gold Account Visa Card... hawa ndio wanatoa huduma bora zaidi kwa wafanyabiashara wa forex nchini

Ushauri wangu kwa wale wanaotaka kufanya Forex
Moja; tambua kwamba forex ni biashara… sio game au sehemu ya kupata utajiri haraka haraka. You need to work hard. Binafsi kuna siku nalala masaa matatu tu (mfano mzuri jana). Kila nikipata muda ambao niko free, yaani siandiki au siko kwenye majukumu mengine, nautumia kufanya analysis, kutafuta good entries, na kujielimisha zaidi kwa kusoma vitabu.
Mbili; Kwa kuwa hii ni biashara hivyo unatakiwa kuelewa kuwa kuna uwezekano ukapata hasara. Kwa hiyo unatakiwa kuiweka saikolojia yako sawa sawa. Hivyo basi unatakiwa kufanyia biashara ya forex fedha ambayo hata ukiipoteza haiwezi kuathiri maisha yako kuendelea kwenye mtiririko. Hivyo basi usitumie karo ya shule ya watoto au ada yako ya chuo au kuchukua mkopo ili ufanye forex. Wako waliofanya hivyo na wakafanikiwa (Mfano Sandile Shezi alitumia karo ya chuo kufund account take ya forex) but its too risk. Sikushauri.
Nimetoa mfano mimi nilipoteza dola 1600 (mtaji niliowekeza ulikuwa dola 320 ambayo ni kama laki saba unusu hivi) japo ni hela nyingi kwa vyuma vilivyokaza lakini bado haijafikia kiwango cha kuathiri mtiririko wa maisha yangu nikiipoteza. Ndio maaana niliipoteza na kisha nikarudi tena.
Tatu; mtu pekee ambaye anaweza kuamua kwamba wewe uwe trader successful au unsuccesful sio Ontario au TMT au JP Markets. Ni wewe mwenyewe. Wewe ndiye mwenye uwezo wa kuamua kama unataka kufanikiwa ndani ya forex au kupoteza hela. Its in your hands.
Nne; usifuate huu mkumbo wa watu, sijui ni mihemuko sijui nini wakianza kupata faida kwenye forex wanasema wanataka kuacha kazi wafocus kwenye forex. KEEP YOUR JOB.!
Listen, hizi hela tunatafuta tu ili kutufanya tuishe kwa fahari na kujitosheleza. Lakini lazima uwe na kitu ambacho kinaku-difine katika maisha. Ni lazima uweke lengo la kuacha legacy fulani hapa duniani. Unaweza kufanya forex na kufanya kazi yako ya siku zote. Kwa hiyo weka bidii na umahiri pia kwenye hicho ambacho unakifanya sasa. Kama ni daktari kuwa mahiri zaidi. Kama ni mwalimu kuwa mahiri zaidi. Kama ni mkulima, lima zaidi.
Kwa mfano mimi niseme kwamba kipato ninachokipata nje ya uandishi ni kikubwa kuliko ninachopata kwenye hii shuguli ya uandishi. Lakini kwa nini naandika?? LEGACY…
Siku mwenyezi Mungu akinichukua nataka Tanzania inikumbuke kama ambavyo tunamkumbuka Shaban Robert na wandishi wengine nguli. Nataka kizazi hicho wakumbuke kwamba aliwahi kuishi muandishi mahiri aliyeitwa The Bold. Ndio maana japo nina shughuli zinazonipa kipato zaidi, lakini shughuli hii ya uandishi naifanya kwa bidii kubwa na kwa umahiri. Sitaki kukumbukwa kama best trader, nataka nikumbukwe kama best writer. Its all about leaving a LEGACY!!
Kwa hiyo fanya forex and Keep your job… unless you hate your job!! Kama huipendi kazi yako unaifanya tu kwa kuwa hauna namna nyingine then i can understand.

Jambo la mwisho nakushauri kwamba… SOMA SOMA SOMA SOMA SOMA. Soma sana na jielimishe kila siku juu ya hii biashara. Jiongezee maarifa kila siku.
Pia hakikisha unakuwa na utulivu wa ndani. Maamuzi sahihi na stategies… and may be One day you and The Bold will be best forex traders in this country.



Hii trade ilikuwa ni juzi... $1,200 profit locked in a day
Jibu la swali ambalo niliulizwa WhatsApp: Hahah chiefs, naomba nijibu hapa kwa faida ya wote (qns kutoka inbox)
Sio kwamba kila siku napata profits za dola elfu moja... hapana (japo wapo wanapata profits za dola elfu moja na zaidi kila siku). But kwangu jana was a BIG DAY with big profits.
Kwa hiyo kuna siku utapata profits za dola mia, kuna siku dola hamsini, siku dola mia mbili, kuna siku unahold tu trades without profits na siku nyingine ndio kama jana, huge profits!! Inategemea ukubwa wa akaunti yako, strategy zako na trading style yako.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog