Posts

Image
VIWANDA VYA KUCHAKATA TAARIFA.?? Kama mtu akikuuliza maswali yafuatayo, unajisi majibu yako yatakuwa ni yapi? 1. Jengo la picha namba moja unahisi linahusiana na nini? 2. Jengo la picha namba mbili ni nyumba ya kuishi au hoteli? Nina amini kabisa majibu mengi yatakuwa kama ifuatavyo… 1. Jengo namba moja ni kiwanda… na inawezekana ni kiwanda kinachohusiana na masuala ya nishati au kemikali. 2. Jengo kwenye picha namba mbili ni aina ya hotel ya nyota tano. Majibu mengi yatakuwa yanafanana na hayo hapo juu na kwa kawaida utakuwa sahihi kabisa… isipokuwa tu hautakuwa umepatia hata nusu ya jawabu. Picha zote mbili ni picha za kituo data (data center). Katika karne ya 18, 19 na 20 wafanyabiashara wenye mitaji mikibwa na makampuji walikuwa wanajenga majengo makubwa ya viwanda. Na wale ambao walikuwa mahiri kwenye uanzishaji na uendeshaji wa viwanda ndio ambao walikuwa wanashamiri kwa kipato na hatimaye kuwa matajiri. Matajiri wote wakubwa wa miaka hiyo… toka kwa wanasa
Image
MAAJABU YA KABILA LA KIKAYAN⠀ Kabila hili linapatikana katika nchi ya MYANMAR wanawake wa kikayan huanza kuvaa bangili shingoni toka Wakiwa wadogo Sana na kadri wanavyo zidi kukua bangili mpya huongezwa⠀ Shingo za wanawake hawa hurefuka kiasi cha kwamba wakizivua kichwa huangukia begani na kuwasababishia kifo bangili hizo huvuliwa chini ya uangalizi wa daktari ⠀ wanaume wa kikayan wao hawaoi mwanamke asiye na bangili shingoni⠀ mpaka sasa hakuna mtu anaye jua utamaduni huu alianzisha Nani na kwa sababu gani Hawa wanawake wameweza kuzitoa bangili kwa msaada wa madaktari.Hapo wakitingishwa kwa nguvu kidogo tu wanakufa. Huyu mtoto ndio kwanza ameanza na bangili chache lakini kadiri anavyokuwa ndio pingili mpya huongezwa. Shingo ikifikia urefu huu huwa misuli yake inalegea kabisa. Gusa hapo chini kutazama video
Image
MAAJABU YA DUNIA:KUTANA NA MAKABURI YA KIFAHARI YANAYOZIDI NYUMBA ZA MATAJIRI...YANA HADI VIYOYOZI  Maishani, watu wengi hutaka kuishi katika nyumba nzuri na za kifahari. Wengi huwa hawafanikiwi. Lakini nchini Mexico, ambapo ulanguzi wa mihadarati umekithiri, wakuu wa magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya huishi maisha ya kifahari, na huendeleza hizi hata wanapokuwa wafu. Nchini humo, utapata makaburi ambayo yangegeuzwa kuwa nyumba, matajiri wengi wangejivunia kuishi.Ni makaburi makubwa yaliyojengwa na kuwekwa huduma za kisasa na vitu vingi vya anasa. Kuna baadhi ya makaburi yenye viyoyozi vya kudhibiti viwango vya joto na kuingiza hewa safi, kuna vioo visivyopenya risasi na baadhi yana hata vyumba ambavyo wageni wanaofika kutoa heshima kwa wafu, wanaweza kuketi na kupata kila kitu kinachopatikana katika nyumba za kifahari. Baadhi yanakadiriwa kugharimu hadi £230,000 (Sh633 milioni za Tanzania; Sh29 milioni za Kenya) Hali hii ni tofauti kabisa kwa maelfu ya watu wanaouawa k
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA SITA Waziri wa fedha Norman Lamont alikwenda moja kwa moja mpaka mahala pa kuzungumza ambako alikuwa ameandaliwa. Muda mchache uliopita alikuwa amemaliza kikao na Waziri Mkuu John Major, Waziri wa mambo ya nje Douglas Hurd, Rais wa Bodi ya Biashara nchini Uingereza Bw. Michael Heseltine na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kenneth Clarke. Alikuwa amefika hapa kutangaza uamuzi ambao ulikuwa umefikiwa na kikao hicho cha dharura. Baada ya waandishi wa habari kutulia, Waziri Lamont kwanza alianza kueleza namna ambavyo kuna hali ya dharura ya kiuchumi ambayo imeikumba Uingereza. Kwamba uchumi umeanza kwenda kombo tofauti na ambavyo walikuwa wanatarajia. Pia alieleza namna ambavyo sarafu yao ilikuwa kwenye msongo mkubwa wa kushindwa kuwezesha biashara kufanyika na kuchochea uwekezaji kutokana na kuonekana thamani yake iko juu zaidi tofauti na uhalisia. Hivyo basi kutokana na Uingereza kuwa ndan
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA TANO "…uwekezaji unahitaji subira. Ni kama vile kupaka rangi nyumba na kusubiri ikauke. Au kupanda mmea na kuusubiri ukue. Kama wewe ni mtu mwenye kupenda furaha ya haraka haraka chukua elfu kumi yako nenda 'coco beach'.!" 'Dili' ya Karne Katika sehemu iliyopita nilieleza namna ambavyo George Soros alianza kutengeneza position yenye thamani ya zaidi ya bilioni 10 za Marekani. Lakini pia tuliangalia kwa mapana maana ya 'short sell' katika soko la hisa na soko la fedha duniani. Katika sehemu hii ya tano twende taratibu hatua kwa hatua tuone namna amnavyo George Soros alishort Paundi ya Uingereza na kuifilisi benki Kuu. Karibu… Usiku wa kuamkia tarehe 16 Septemba 1992 wakati ambao ulimwengu mzima umelala George Soros kupitia Quatumn Fund alikuwa anaazima na kuuza Paundi ya Uingereza kuzidi katika kiwango kikubwa na cha kutisha. Alikuwa anaazima ku
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA NNE "…haina maana kusema kuwa unajiamini alafu unaogopa ufanya vitu hatarishi…" Nilieleza katika sehemu ya pili ya mfululizo wa makala hii kwamba, siku zote soko la dunia la fedha huwa linainfluence exchange rate ya sarafu husika. Kwa hiyo serikali ambayo imeamua kuweka fixed exchange rate mara nyingi wanajikuta wanaingia kwenye mtego wa kushiriki kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida katika soko ili kuhakikisha kwamba kiwango walichokiweka kinabakia pale pale. Lakini kuna msemo wanasema kwamba ukweli una tabia ya kutopendwa kupuuzwa. Lakini pia hata ukijenga ukuta imara kiasi gani, hauwezi kuyazuia mafuriko milele, iko siku na saa ambayo hautatarajia ukuta huo utadondoshwa na nguvu ya mafuriko. Kilichowapata Uingereza kwa kiasi fulani kilikuwa kinafanana kabisa na hiki. Mpaka kufikia mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka 1992, hali ya ndani kwa ndani serikali kulikiwa na kia
Image
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA TATU Katika sehemu iliyopita nilieleza namna ambavyo nchi ya Uingerrza iliingia katika mpango wa ERM baada ya uchumi wao kudorora. Lakini pia nilieleza namna namna ambavyo hali ya kiuchumi ilianza kutengemaa mara tu baada ya Uingereza kuwa chini ya mpango wa ERM. Nikaeleza kwa kwa ufupi pia ni namna gani ambavyo George Soros alikuwa anaona anguko kubwa la sarafu ya Paundi tofauti na watu wengi ambavyo walikuwa wanaona kutengemaa na kushamiri kwa uchumi wa Uingereza. Kabla sijaingia ndani kueleza ni namna gani ambavyo George Soroa aliweza kutumia fursa ya dirisha ambalo aliliona katika anguko la uchumi wa Uingereza ni vyema kwanza kumuelewa hata kidogo George Soros ni nani. Tukielewa japo kwa uchache George Soros ni nani itatusaidia kuelewa saikolojia yake ya Biashara na namna ambavyo aliweza kuipigisha magoti nchi ya Uingereza mwaka 1992 na mwishoni mwa miaka ya 1990s alivyochochea anguko