UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY HITIMISHO Kama ambavyo nilieleza asubuhi kwamba nitahitimisha makala hii kwa maneno machache sana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu ambazo zilinifanya hata kukatisha muendelezo wa makala hii siku zilizopita. Lakini naamini tutakuwa tumefikia lengo. Tuendelee… Katika ripoti ya The Warren Commision, ile kamisheni iliyoundwa na Rais Lyndon B. Johnson kuna mahala inasema kwamba kuna mtu ambaye alijitambulisha kama "Clay Bertrand" alimpigia simu Dean Andrews Jr. ambaye alikuwa ni mwanasheria wa kujitegemea kwenye jimbo la New Orleans kumtaka apande ndege kwenda Dallas kumtetea Lee Harvey Oswald. Lakini wajumbe wa Warren Commision wanadai kwamba walihangaika mno bila mafanikio na hawakujua huyu "Clay Bertrand" ni nani na wakafanya hitimisho kwamba hili halikuwa jina halisi bali ni 'alias' ambayo ilitumiwa tu na huyo mtu. Ilipofika mwaka 1967 mwezi March… mwanasheria wa serikali wa New Orleans wa kipindi hi...