BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA SEHEMU YA SITA Waziri wa fedha Norman Lamont alikwenda moja kwa moja mpaka mahala pa kuzungumza ambako alikuwa ameandaliwa. Muda mchache uliopita alikuwa amemaliza kikao na Waziri Mkuu John Major, Waziri wa mambo ya nje Douglas Hurd, Rais wa Bodi ya Biashara nchini Uingereza Bw. Michael Heseltine na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kenneth Clarke. Alikuwa amefika hapa kutangaza uamuzi ambao ulikuwa umefikiwa na kikao hicho cha dharura. Baada ya waandishi wa habari kutulia, Waziri Lamont kwanza alianza kueleza namna ambavyo kuna hali ya dharura ya kiuchumi ambayo imeikumba Uingereza. Kwamba uchumi umeanza kwenda kombo tofauti na ambavyo walikuwa wanatarajia. Pia alieleza namna ambavyo sarafu yao ilikuwa kwenye msongo mkubwa wa kushindwa kuwezesha biashara kufanyika na kuchochea uwekezaji kutokana na kuonekana thamani yake iko juu zaidi tofauti na uhalisia. Hivyo basi kutokana na Uingereza kuwa ndan...